Wajumbe wa Serikali za Mitaa wanaendelea kudharauliwa na kutokuthaminiwa
Wajumbe wa serikali za mitaa wamelalamikia Bajet iliyosomwa na Mh Meya wa mansipaa ya kinondon Mh Bonfas Jacob kuwa haikutekelezwa kama ambavyo alisema katika bajeti hiyo, Meya alisema ni matusi makubwa kwa wajumbe wa serikali ya mtaa kulipwa posho ya 5000.
Lakini alikwenda mbali zaidi kwa kusema matusi hayo yanazidi pale ambapo mjumbe anapokea hiyo posho. Sasa cha kushangaza mara baada ya kuaza kwa bajeti hiyo wajumbe wameendelea kupewa hiyo hiyo Tsh 5,000 isipokuwa Wenyeviti na Madiwani posho zao zimekwenda kama alivyo ahidi.
Sasa wajumbe hawa wanataka kujua Mh Meya na yeye ameamua kuendeleza matusi yale yale ambayo aliyapinga kwa msisitizo?
Hivi umuhimu wa wajumbe katika serikali hizi nini hasa ? Na hata baada ya posho hizo za wenyeviti kupanda bado maeneo mengine wajumbe hawajalipwa hadi leo na pesa zao zimeliwa na maafisa watendaji kata mfano wa mtaa wa Mtambani hadi leo wajumbe hawajalipwa huku manispaa ikionyesha pesa hizo zimefika. ivi umakini wa usmamizi wa pesa za manspaa uko wapi ?....

Comments
Post a Comment