Kama Unafikiri Umeshindwa Na Hauwezi Tena Basi Hii Ni Habari Njema Juu Ya Kushindwa Kwako


Mara nyingi tumekuwa tukipanga kufanya mambo mengi sana mengine tunafanikiwa na mengine yanashindikana. Tunapata furaha sana pale tunapofanikiwa na mara nyingi huwa tunaumia sana pale tunaposhindwa.

Sasa kama wewe umeshindwa kila mara na unaona sasa imetosha huwezi kujaribu tena naomba nikupe habari hii nzuri kuwa kushindwa ni mojawapo ya hatua za kufikia mafanikio ila kama tu utaona kushindwa kwako sio mwisho wako.

THUBUTU KUJARIBU TENA NA TENA NA TENA.....

Inawezekana ulifikiria kufanya biashara yako kwa namna fulani lakini matokeo hayakuwa kama ulivyo tarajia, au kusoma masomo fulani lakini hukufikia mafanikio uliyojiwekea, au kufanya kitu kingine chochote kile lakini matokeo yakawa tofauti.

Tumezoea katika jamii yetu wale wanaofanikiwa tu ndio wanaosifiwa. Wale wanaojaribu na kushindwa huwa ndio mfano wa kuwakatisha tamaa wale wenye ndoto za kufikia mafanikio. Lakini usiogope kwakua kushindwa kwako leo, ndio mafanikio yako kesho.
Kwanini nasema hivi.

Pale unapojaribu na kushindwa sio rahisi wewe kushindwa tena wakati mwingine kwa kigezo kile kilichosababisha ushindwe mara ya kwanza. Unapoendelea na safari yako ya mafanikio utakuwa makini na yale maeneo ambayo hayakuenda vizuri na kurekebisha ili kuzuia makosa ya awali kujitokeza tena. Kwa hiyo faida yake hapo ni kuwa na uzoefu.

Unaposhindwa unapata nafasi ya kupanua akili yako na kufikiri kwa ukubwa zaidi. Kwa kufikiri zaidi unaweza kupata kitu kipya kikubwa ambacho kitakuwa chanzo cha mafanikio yako.

Unachotakiwa kufanya pale unapoona umeshindwa sio kukata tamaa, ni kuangalia wapi ulikosea, kurekebisha na kusonga mbele. Kwa kukosea tunakua imara zaidi na tunafanya mambo kwa umakini zaidi. Lakini hii haina maana ukosee kwa kukusudia. Ukikosea kwa kukusudia ni dalili za uzembe. Na kwa kuwa mzembe mafanikio huwezi kupata..

Endelea kuongeza juhudi na maarifa katika kile unachokifanya. Usiogope kushindwa ni njia mojawapo ya kujifunza. Lakini tumia uwezo ulionao kutatua changamoto zozote unazokutana nazo na utafikia mafanikio.

Comments

Popular posts from this blog

UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI

YANGA YAPATA PIGO, KIPA WAKE NAMBA MOJA DEO MUNISHI AFIWA NA BABA YAKE

Kwa Nini Watu Wengi Wanaamini Uchawi Unaleta Mafanikio?