NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI ANAYESHUGHULIKIA MASUALA YA AFRIKA


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Linda Thomas-Greenfield walipokutana wakati wa Mkutano wa TICAD VI Jijini Nairobi na kuzugumzia masuala ya ushirikiano.

Wakati wa mazungumzo hayo Mhe. Dkt. Kolimba alimshukuru Mhe. Greenfield kwa ushiriano uliopo kati ya Tanzania na Marekani ambapo nchi hiyo imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika kuboresha huduma za afya na miradi mingine ya maendeleo.


Mhe. Naibu Waziri akizungumza na Mhe. Greenfield.

Mhe. Dkt. Susan aiagana na mgeni wake Mhe. Greenfield mara baada ya mazungumzo huku Bi. Makilagi (katikati) akishuhudia.

Mhe. Naibu Waziri (mwenye gauni la bluu) akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Bi Talha Waziri (wa pili kutoka kulia), Bw. Adam Isara, Msaidizi wa Naibu Waziri na Bi. Bertha Makilagi (kushoto), Afisa Mambo ya Nje.

Comments

Popular posts from this blog

UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI

YANGA YAPATA PIGO, KIPA WAKE NAMBA MOJA DEO MUNISHI AFIWA NA BABA YAKE

Kwa Nini Watu Wengi Wanaamini Uchawi Unaleta Mafanikio?