Posts

Showing posts from August, 2016

Tanzania yanufaika na miradi ya ICF

Image
Tanzania ni moja ya nchi zilizonufaika na uwezeshaji ambao umekuwa ukitekelezwa na taasisi inayojishughulisha na uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji barani Afrika ya Investment Climate Facility – ICF. Moja ya malengo ya taasisi hiyo imeelezwa kuwa ni kuona nchi za Afrika zinasimamia zednye mipango ya kukuza uchumi na uwekezaji. Mwenyekiti Mwenza wa Taasisi hiyo, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mzee Benjamin William Mkapa, amesema hayo katika mkutano na wanahabari jijini Dar es Salaam hii leo, mkutano ambao lengo lake ni kutoa ripoti ya mafanikio yaliyopatikana na ICF tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007. Rais Mstaafu Mkapa ametaja baadhi ya maeneo ambayo Tanzania imenufaika kutokana na kuwa nchi mwanachama wa ICF kuwa ni maboresho katika usajili wa biashara, uwazi na ufanisi katika mfumo wa forodha, maboresho katika sheria na taratibu za kodi pamoja na mfumo bora wa kisheria wa utatuzi wa migogoro ya kibiashara ambayo kwa ujumla wake imesaidia kuchochea kasi ya ukuaji

RC Arusha Mrisho Gambo aendelea na ziara yake ya kujitambulisha kwa viongozi wa dini jijini Arusha leo

Image
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameendelea  na  ziara yake ya kujitambulisha kwa viongozi wa dini  ukiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na viongozi  baada ya kuteuliwa kushika  wadhifa huo hivi karibuni. Mh.Gambo amekutana na  Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dayosis ya Kaskazini Kati, Mchungaji  Solomon Masangwa , Askofu wa  Kanisa la Evangelistic Assemblies of God(EAGT) mkoa wa Arusha,Leonard Mwizarubi  na Askofu  Stanley Hotay wa Kanisa la Anglikana , Dayosisi ya Mount  Kilimanjaro. Katika mazungumzo na viongozi hao kwa nyakati tofauti mbali na kujitambulisha aliwahakikisha dhamira ya serikali kulinda na kuheshimu uhuru na haki ya kuabudu ambayo imekuwepo nchini kwa muda mrefu ikiwa ni njia ya kuwa na taifa la watu wenye hofu ya Mungu. Alisema kutokana na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Joseph Pombe Magufuli kutaka kuwainua wananchi wa chini kupitia mapato ya ndani  halmashauri zimetenga asilimia 10 kutoka kwenye mapato ya

Kipaombele changu sasa siyo uchaguzi ujao - Bulaya

Image
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia tiketi ya CHADEMA Ester Bulaya amesema kipaombele chake kwa sasa siyo uchaguzi ujao wa 2020, bali ni kuwatumikia wananchi wa jimbo lake na kutimiza ahadi zake. Bulaya pia amesema kuwa wananchi wa jimbo lake watampima kutokana na namna anavyofanya kazi za kuwatumikia kulingana na ahadi ambazo aliahidi. Akizungumza katika kipindi cha HOTMIX kinachorushwa na EATV, Bulaya amesema mara baada ya kuchaguliwa na wananchi wa Bunda ameweza kusaidia mchakato wa kutatua kero mbalimbali za wananchi kama ujenzi wa zahanati, ujenzi wa bweni, ujenzi wa madarasa, miradi ya maji, madawati mashuleni pamoja na kugawa vifaa vya michezo kwa vijana ili waweze kushiriki michezo. “Jimbo langu lina changamoto kubwa sana za huduma za kijamiii, nimeanza kukabiliana nazo kwa kuhakikisha kila senti tunayopata kwa ajili ya maendeleo inatumika kama ilivyokusudiwa, na katika ubunge wangu mara nyingi ninashinda jimboni ili kuhudumia wananchi kama nilivyoahidi” Amesema Bulaya.

UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI

Image
SEHEMU YA KWANZA UTANGULIZI Napenda kumshukuru mwenyezi Mungu ambaye ameniwezesha kwa namna moja au nyingine kutoa mchango wangu kwa mtindo huu. Huu ni kama mwongozo tu wa nini utakabiliana nacho au unatakiwa kufanya katika zoezi zima la ufugaji wa kuku wa kienyeji. Nimeamua kuuleta kwenu ili kwa mtu mwenye malengo ya kufanikiwa kupitia ufugaji wa kuku ajue mlolongo mzima na changamoto ambazo atakabiliana nazo. A.KWA NINI KUKU WA KIENYEJI? 1. Wastahimilivu wa magonjwa lakini ni muhimu wakikingwa na magonjwa ya kuku kama mdondo, ndui ya kuku n.k ili kuweza kuwaendeleza. 2. Wana uwezo wa kujitafutia chakula ardhini. 3. Wana uwezo wa kuatamia mayai, kutotoa na kulea vifaranga na ustahimilivu wa mazingira magumu kama ukame, baridi n.k 4.Nyama na mayai yake vina ladha nzuri kuliko kuku wa kisasa.( PATA SUPU YA KUKU WA KIENYEJI ILI UTHIBITISHE) 5. Wana uwezo wa kujilinda na maadui kama mwewe n.k . Pamoja na sifa hizi ni muhimu muhimu kuku hao wakapewa matunzo mazuri, wakawekwa kwenye mab

UBONGO WA MTU UNA SELI 100 BILLIONI ZA MAWASILIANO

Image
Ubongo una mfumo wa mawasiliano ya kustajabisha kama makala haya yanavyochambua. Ubongo ni kiungo cha aina yake katika mwili wa binadamu. Ubongo hutoa kila fikira, tendo, kumbukumbu, hisia na uzoefu wa kidunia. Kwa mujibu wa jarida la New Scientist, Ubongo wa binadamu umetengenezwa na viini laini vilivyo katika mfumo kama mafuta mazito yaliyoganda. Ubongo umegawanyika katika sehemu tatu, ya mbele, kati na ya nyuma. Sehemu hizi zinazofanya kazi kwa pamoja japo kila sehemu ina viini vinavyofanya kazi za kipekee katika mwili. Jarida la Live Science la Mei 6, 2013 linabainisha kuwa ubongo wa binadamu ni mkubwa kuliko ubongo wa kiumbe kingine kwa uwiano wa ukubwa wa mwili. Ubongo wa binadamu una uzito wa kilo 1.4 sawa na paundi tatu ama gramu 1,300 hadi 1,400 wenye seli za mawasiliano (neurons) bilioni 100 ambazo ndani yake maagizo ya ubongo hupitia kwa kasi katika mfumo wa mapigo au kama msukumo wa umeme. Msukumo huu husafiri kwa kasi ya zaidi ya kilometa 400 kwa saa. Ubongo hutoa na k

Klabu ya Stoke City imemsajili mshambuliaji Wilfried Bony kwa mkopo kutoka Manchester City.

Image
Klabu ya Stoke City imemsajili mshambuliaji Wilfried Bony kwa mkopo kutoka Manchester City. Raia huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 27,ameanzishwa mara 15 tangu ajiunge na City kwa kitita cha pauni milioni 28 kutoka Swansea mnamo mwezi Januari 2015 , lakini hajacheza chini ya mkufunzi mpya Pep Guardiola. Stoke pia imemsajili kipa wa Derby, Lee Grant mwenye umri wa miaka 33 kwa mkopo hadi mwezi Januari. Wakati huohuo Beki wa Porto na Uholanzi Bruno Martins Indi mwenye umri wa miaka 24 anaendelea na mazungumzo ya kusajiliwa na klabu hiyo.

Kama Unafikiri Umeshindwa Na Hauwezi Tena Basi Hii Ni Habari Njema Juu Ya Kushindwa Kwako

Image
Mara nyingi tumekuwa tukipanga kufanya mambo mengi sana mengine tunafanikiwa na mengine yanashindikana. Tunapata furaha sana pale tunapofanikiwa na mara nyingi huwa tunaumia sana pale tunaposhindwa. Sasa kama wewe umeshindwa kila mara na unaona sasa imetosha huwezi kujaribu tena naomba nikupe habari hii nzuri kuwa kushindwa ni mojawapo ya hatua za kufikia mafanikio ila kama tu utaona kushindwa kwako sio mwisho wako. THUBUTU KUJARIBU TENA NA TENA NA TENA..... Inawezekana ulifikiria kufanya biashara yako kwa namna fulani lakini matokeo hayakuwa kama ulivyo tarajia, au kusoma masomo fulani lakini hukufikia mafanikio uliyojiwekea, au kufanya kitu kingine chochote kile lakini matokeo yakawa tofauti. Tumezoea katika jamii yetu wale wanaofanikiwa tu ndio wanaosifiwa. Wale wanaojaribu na kushindwa huwa ndio mfano wa kuwakatisha tamaa wale wenye ndoto za kufikia mafanikio. Lakini usiogope kwakua kushindwa kwako leo, ndio mafanikio yako kesho. Kwanini nasema hivi. Pale unapojaribu na kushind

TRL yatangaza nauli mpya treni ya Pugu

Image
NAULI  ya abiria wa treni inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Pugu jijini Dar es Salaam, imepanda kutoka Sh 400 ya awali hadi 600. Tozo hiyo ya nauli mpya inatarajiwa kuanza rasmi Septemba mosi, mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Ng’hwani Kudema, alisema viwango hivyo vya nauli vilivyokokotolewa na Mamlaka ya Majini na Nchi Kavu (Sumatra), vimepanda kutokana na gharama za uendeshaji kuwa juu. “Baada ya siku 14 nauli hizi zitaanza kutozwa kwa mujibu wa utaratibu na hili tutabandika matangazo. Hadi kufikia Septemba 13, mwaka huu nauli itakayokuwa inatozwa ni shilingi 600 kwa mtu mzima na shilingi 100 kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari,” alisema Kudema Alisema wakati wa majaribio ya treni hiyo Agosti mosi, mwaka huu, walikuwa na mabehewa 10 lakini kutokana na mahitaji ya usafiri huo kuwa mkubwa, walilazimika kuongeza mabehewa ambayo kwa sasa yamefika 18.

Shule nyingine yaungua moto Manyara

Image
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Manyara, Francis Massawe. MATUKIO  ya kuteketea kwa moto mabweni ya wavulana katika shule za sekondari zilizoko Kanda ya Kaskazini yanazidi kushika kasi. Juzi, moto uliteketeza bweni la Shule ya Sekondari ya Wavulana Aldersgate, iliyopo wilayani Babati, Mkoa wa Manyara. Kuteketea kwa bweni hilo ni mwendelezo wa matukio ya aina hiyo baada ya shule kadhaa kuteketea katika mikoa ya Arusha na Manyara. Tukio la hivi karibuni ni la Shule ya Sekondari Mulbadaw iliyopo wilayani Hanang, ambayo mabweni yake yaliteketea kwa moto na kuharibu mali zote za wanafunzi shuleni hapo. Katika tukio la Shule ya Sekondari ya Wavulana Aldersgate, moto ulitokea juzi saa tatu usiku wakati wanafunzi wakiwa madarasani. Hata hivyo, taarifa zilizopatikana kutoka kwa walimu na wanafunzi ambao hawakutaka kutaja majina yao, zinasema inawezekana chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme. Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Manyara, Francis Massawe, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema

Messi kukosa mechi dhidi ya Uruguay

Image
Kambi ya Argentina imethibitisha kuwa Messi, mwenye miaka 29, anasumbuliwa na maumivu ya misuli ya pajani ambayo aliyapata Jumapili iliyopita wakati klabu yake FC Barcelona iliifunga Athletic Bilbao 1-0 kwenye La Liga huko Uhispania. Hadi sasa haijajulikana iwapo Messi atacheza mechi zao mbili za kufuzu kombe la Dunia za Ijumaa dhidi ya Uruguay itakayochezwa huko Mendoza, Argentina na ile inayofuatia ya ugenini huko Merida dhidi ya Venezuela siku 5 baadae. Messi alijiuzulu kuichezea Argentina mwezi Juni baada ya kushindwa fainali ya Copa America walipobwagwa na Chile lakini baada ya kocha mpya Edgardo Bauza kuteuliwa nahodha huyo wa nchi yake aligeuza uamuzi wake. Mechi hizo za Argentina zitakuwa chini ya kocha wao mpya Edgardo Bauza kwa mara ya kwanza ambazo pia atawakosa washambuliaji wa Man City Sergio Aguero na kiungo wa Paris St Germain Javier Pastore kwani wote wamejiondoa kikosini kutokana na kuumia. Nao, Vigogo wengine wa Marekani ya Kusini, Brazil, chini ya kocha mpya Tite

Waendesha Bodaboda washauriwa kutochanganya kazi na siasa

Image
  Mwenyekiti wa  Muungano wa Vyama vya Waendesha Bodaboda Dar es Salaam Bw. A. Leonard Mdede (wapili kutoka kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu waendesha Bodaboda kutojihusisha na mamandamano ya UKUTA leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Michael Maiko, Mapinduzi Mpema na Said Kagambo. Katibu wa  Chama cha Waendesha Bodaboda Wilaya ya Kinondoni (KIDITIMA)  Oscar Waluye (katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuhusu waendesha Bodaboda kutojihusisha na mamandamano ya UKUTA uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari, MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni  Mwenyekiti wa  Muungano wa Vyama vya Waendesha Bodaboda Dar es Salaam Bw. Mdede,Said Kagambo,Mapinduzi Mpema na Michael Maiko ambao ni viongozi wa vyama hivyo. VIONGOZI wa madereva waendesha bodaboda mkoa wa Dar es salaam wamewaasa wanachama wao kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ya nchi kwa manufaa ya Watanzania wote. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti

Alichokisema aliyekuwa katibu wa chadema mkoani Mwanza baada ya kutimkia CCM

Image
 Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mkoani Mwanza, John Nzwalile (kulia), akirejesha kadi ya chama hicho kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mwanza, Dkt.Anthony Diallo katika ofisi za CCM hii leo. Nzwalile ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema Taifa, Mjumbe Baraza Kuu Chadema Taifa, Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano Chadema Mkoa wa Mwanza, amefikia uamuzi huo baada ya jana kujivua vyeo hivyo. Amesema amefikia hatua hiyo kutokana na kwamba Chadema imepoteza mwelekeo kwani kimekuwa kikiibuka na oparesheni za kuichonganisha serikali na wananchi huku pia demokrasia ikikosekana ndani ya chama hicho. "Kama ni udikiteta basi mimi niseme Chadema ndiko kuna udikiteta kwani zaidi ya mara tatu nimemsikia Lowasa (Edward Lowasa, aliyekuwa mgombea urais 2015) akisema yeye ndiye mgombea urais mwaka 2020, kwa kikao gani". Amesema Nzwalile na kuongeza kwamba yale mambo yote mabaya yaliyokuwa yakifanyika ndani ya CCM yamenyooshwa hivyo

Jack Wilshere kujiunga na Bournemouth

Image
Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere anakaribia kujiunga na klabu ya Bournemouth kwa mkopo wa muda wa msimu uliosalia baada ya mpango wa kuijiunga na klabu ya Roma kuzuiwa na Arsenal. The Gunners ilikataa kufanya biashara na Roma kwa sababu ya vile walivyochukulia uhamisho wa beki Kostas Manolas mapema msimu huu. Wilshere mwenye umri wa miaka 24 alifanya mazungumzo na Bournemouth na Crystal Palace. Anatarajiwa kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu na The Cherries.

Samir Nasri ajiunga na Sevilla ya HIspania kwa mkopo toka Man City

Image
Manchester City wamethibitisha kiungo mshambuliaji wao Samir Nasri kujiunga na Sevilla kwa mkopo wa msimu mzima. Awali iliripotiwa kwamba, Nasri angejiunga na miamba ya Uturuki Besiktas, lakini mwishoni kabisa Sevilla wameonekana kuwa na mkono mrefu zaidi. Mkurugenzi wa Ufundi wa Sevilla Monchi ametanabaisha kwamba, Nasri ni mchezaji ambaye wamekuwa wakimfukuzia kwa muda wote kwenye dirisha hili la usajili. Mkataba huo wa mkopo hauna kipengelea cha Nasri kununuliwa moja kwa moja endapo Sevilla watahitaji kufanya hivyo.

Kwa Nini Watu Wengi Wanaamini Uchawi Unaleta Mafanikio?

Image
Katika wiki mbili zilizopita tuliona uhusiano kati ya uchawi na mafanikio na pia kwa nini waganga wanaweza kuwasaidia wengine kuwa matajiri wakati wao ni masikini. Katika makala hizi tuliona ni jinsi gani hata wewe unaweza kutumia mbinu hizo za kisaikolojia bila hata ya kuwa mchawi na ukaweza kufikia mafanikio makubwa. Kama hukupata nafasi ya kusoma makala hizo bonyeza hizo link kuzisoma. Leo tutajadili kwa nini watanzania wengi wanaamini uchawi unaleta mafanikio. Kwa nini tunashuhudia mauaji ya vikongwe na albino yakiendelea? Kwa nini kila siku tunaona mabango ya waganga wakijinadi kuweza kuwapatia watu utajiri na bahati? Na kwa nini kwenye jamii kila anayeonekana kuwa na mafanikio makubwa anaambiwa ni freemason? Kuna sababu kubwa tano zinazosababisha watu wengi kuamini kwenye uchawi na ushirikina. 1. Mila na desturi. Katika makabila mengi ya kitanzania kwa muda mrefu kumekuwa na mila ambazo watu hufanya ibada tambiko. Pia makabila mengine yana asili ya imani hizi za uchawi hivy

Waliochuma watumishi hewa kikaangoni

Image
SERIKALI imeanza kuwashughulikia watumishi walionufaika na fedha za watumishi hewa ambapo hadi sasa watumishi 839 wapo katika hatua mbalimbali wakiwemo waliofikishwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na wengine wanaendelea kuhojiwa polisi kwa ajili ya kufikishwa mahakamani. Sambamba na hilo, serikali inatarajia kutoa ajira mpya 71,496 kwa mwaka huu wa fedha baada ya kukamilisha uondoaji wa wafanyakazi hewa. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angella Kairuki aliyasema hayo wakati akizungumzia utekelezaji wa mipango na mikakati ya wizara yake katika kipindi cha ‘Tunatekeleza’ kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1). Kairuki alisema, “Kwa sasa tayari wapo watumishi wameshahojiwa na kuchukuliwa maelezo yao polisi na upelelezi utakapokamilika watachukuliwa hatua mbalimbali za kisheria, ikiwemo kufikishwa mahakamani… Tunakamilisha ushahidi na tutawatangazia tutakapokamilisha,” alisema. Alisema waligundua kwamba kuna maofisa utumis

JITIBU MAGONJWA MBALIMBALI KWA KUNYWA MAJI YA UVUGUVUGU-2

Image
Maradhi ya muda mrefu na mfupi yanayosababisha vifo, yanaweza kupona kwa njia rahisi sana.  Njia hii si nyingine bali ni maji ya kunywa. imeelezwa na wataalamu kwamba mtu anaweza kujitibu maradhi ya muda mrefu na mfupi kama haya yafuatayo:- Kuumwa kichwa (headache), shinikizo la damu (BP), upungufu wa damu (Anaemia), kupooza, unene (obesity), mapigo ya haraka ya moyo na kuzimia. Kikohozi, kuumwa na koo (Bronchitis), pumu na kifua kikuu (TB), kiungulia, kuharisha, kufunga choo na kisukari (Diabetes).Mengine ni pamoja na matatizo yote ya macho. Matatizo ya kike kubadili siku zao, kansa ya kizazi, magonjwa ya pua, masikio na koo. NAMNA YA KUTUMIA: Amka asubuhi na mapema.  Kabla hujapiga mswaki na kunawa uso, kunywa maji kiasi cha bilauri nne (4). Kisha unaweza kunawa na kupiga mswaki. Baada ya hapo usinywe chai au kula chochote mpaka zipite dakika arobaini (40).  Baada ya kunywa chai kaa masaa mawili (2), kunywa maji bilauri nne (4),  kaa dakika arobaini (40) kabla ya kula chochote.