Wakusanya ushuru wailiza halmashauri
Handeni. Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, inapoteza zaidi ya Sh 240 milioni kwa mwaka kutokana na mawakala kushindwa kuwasilisha kiwango cha ushuru walichokubaliana kukusanya katika mikataba.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ramadhani Dilliwa alisema kutokana na kukiuka mkataba huo, ilitarajia kuanza kukusanya ushuru huo juzi.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo, Dilliwa alisema uamuzi huo utasaidia kuokoa fedha nyingi zinazopotea.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, Abdallah Pendeza alisema halmashauri inakabiliwa na changamoto ya kukosa mapato kutoka kwa wazabuni.

Comments
Post a Comment