Wakala wa Yaya Toure amvaa Guardiol
Toure, ambaye aliondoka Barcelona iilyokuwa chini ya Guardiola mwaka 2010 na kuhamia Man City, amebaki Etihad baada ya dirisha la usajili kufungwa rasmi na hivyo hana nafasi tena ya kushiriki Michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa.
Mpaka sasa chini ya Guardiola, Toure amecheza mechi moja ya kuwania kufuzu kucheza makundi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Steaua Bucharest, hivyo wakala wake Dimitri Seluk. anaona ni wakati sahihi kwa mchezaji huyo kuondoka kwenye dirisha la usajili mwezi January.
“Kama atachukua taji la Ligi ya Mabingwa msimu huu, basi nitasafiri mpaka England na nitasema mbele ya runinga kwamba Pep Guardiola ni meneja bora kabisa duniani,” Seluk alinukuliwa na gazeti la Sunday Mirror.
“Lakini kama City hawatashinda Champions League basi naamini Pep atapaswa kusema wazi kwamba hakuwa sahihi kumfanyia unyama mchezaji mkubwa wa kaliba ya Yaya.
“Haya ni maamuzi ya Pep na tunapaswa kuyaheshimu. Yaya ni mchezaji mwenye weledi na hivyo basi anafanya kila kitu ambacho anaelekezwa kufanya.
Pengine Pep ataona kwamba anafaa kucheza dakika 10 za mwisho za mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya timu ya daraja la tatu….ndiyo, natania tu lakini.
“Lakini ninachoweza kukwambia ni kwamba Yaya atacheza msimu wote hapa Man City. Hataondoka katika dirisha la usajili la mwezi Januari. Anaamini kwamba bado atapata fursa ya kuthibitisha ubora alionao.”
Comments
Post a Comment