Ubongo una mfumo wa mawasiliano ya kustajabisha kama makala haya yanavyochambua. Ubongo ni kiungo cha aina yake katika mwili wa binadamu. Ubongo hutoa kila fikira, tendo, kumbukumbu, hisia na uzoefu wa kidunia. Kwa mujibu wa jarida la New Scientist, Ubongo wa binadamu umetengenezwa na viini laini vilivyo katika mfumo kama mafuta mazito yaliyoganda. Ubongo umegawanyika katika sehemu tatu, ya mbele, kati na ya nyuma. Sehemu hizi zinazofanya kazi kwa pamoja japo kila sehemu ina viini vinavyofanya kazi za kipekee katika mwili. Jarida la Live Science la Mei 6, 2013 linabainisha kuwa ubongo wa binadamu ni mkubwa kuliko ubongo wa kiumbe kingine kwa uwiano wa ukubwa wa mwili. Ubongo wa binadamu una uzito wa kilo 1.4 sawa na paundi tatu ama gramu 1,300 hadi 1,400 wenye seli za mawasiliano (neurons) bilioni 100 ambazo ndani yake maagizo ya ubongo hupitia kwa kasi katika mfumo wa mapigo au kama msukumo wa umeme. Msukumo huu husafiri kwa kasi ya zaidi ya kilometa 400 kwa saa. Ubongo hutoa na k...
Comments
Post a Comment