Posts

Showing posts from September, 2016

Dalili Ya Ng'ombe Mwenye Afya

Image
 Ng'ombe mwenye afya kwa kawaida pua yake huwa na unyevu unyevu au kama vile inatoa jasho jembamba sana.Ukiona ng'ombe wako ana pua iliyokauka na haina unyevuunyevu basi ujue hiyo ni dalili kwamba kuna tatizo katika mwili wake, hii inaweza pia kuwa dalili ya maambukizi au magonjwa  Pua ya ng'ombe inauwezo wa kunusa umbali wa kilometa 8 au maili 5, ndio maana wanaweza kukimbia machungoni au hata kuvunja banda na kufuata mazao mashambani sababu ya harufu, msimu wa membe tatizo la kutoroka ndio huwa kubwa hasa maembe yapaoanza kuiva Kwa siku hutumia masaa 6 kula chakula na hutumia masaa 8 kucheua na na kutafuna tena na hunywa maji kiasi cha lita 12 mpaka 25 kutegemeana na ukubwa na hula kiasi cha kilo mpaka 45 kwa ng'ombe wakubwa Ng'ombe mwenye kilo 1000 huweza kuzalisha kiasi cha tani 10 za mbolea kwa mwaka Ng'ombe aina ya friesian (pichani juu)ambao ni kinara wa uzalishaji wa maziwa duniani wana rangi nyeupa na mabaka meusi ambapo haya mabaka

Picha: Vijana 30 kutoka nchi 5 waingia kwenye kijiji cha Maisha Plus

Image
Masoud na Babu wa Kijijini wakiteta jambo  Vijana 30 kutoka nchi tano za Afrika Mashariki, Jumapili hii waliingia rasmi kwenye kijiji cha shindano la Maisha Plus. Kuwasili kwa vijana hao katika kijiji hicho ambacho hakijulikani kilipo, kulikuwa kukirushwa live kupitia kituo cha runinga cha Azam Two. Wakiwa na mabegi yao mkononi, washiriki hao walipokelewa na mwanzilishi wa kipindi hicho, Masoud Kipanya huku wakiwa wamefunikiwa vitambaa vyeusi machoni. Babu akikagua himaya yake Mshindi wa shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 30. Washiriki wote watapewa shilingi 7,000 kwa wiki ili kujikimu wakiwa kwenye kijiji hicho kilichopo katikati ya msitu. Lengo la kupewa shilingi 1,000 kila siku ni kuwafunza maisha ya waafrika wengi ambao huishi chini ya dola moja kwa siku. Hakuna nyumba kwenye kijiji hicho na hivyo watatakiwa kujenga nyumba zao wenyewe za kuishi. Tazama picha zaidi hapo chini.  Washiriki wakiwa wamefunikwa vitambaa vyeusi usoni mwao  Babu akim

Orodha mauaji dada’ke Bilionia Msuya yaongezeka

Image
Marehemu Aneth Msuya .  Dar es Salaam.  Idadi ya washtakiwa katika kesi ya mauaji ya Aneth Msuya ambaye alikuwa dada wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Erasto Msuya maarufu bilionea Msuya, imeongezeka na kufikia wawili baada ya mwingine kuunganishwa nayo. Awali, Agosti 23, mwaka huu mshtakiwa Miriam Mrita (41) ambaye ni mke wa bilionea huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth aliyekuwa wifi yake. Hata hivyo, juma moja baadaye, mfanyabiashara wa jijini Arusha, Revocatus Evarist (40),  alipandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo na kuuunganishwa na Miriam kwenye kesi hiyo. Evarist alipandishwa kizimbani mahakamani hapo Ijumaa iliyopita na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo.

Picha 10: Dereva wa Kirikuu Anusurika Kifo Baada ya Gari Lake Kuwaka Moto

Image
 Gari lilivyowaka.  Mashuhuda  Mashuhuda.  Dereva wa gari hilo, Michael Augustino akitoa taarifa kwa bosi wake.  Michael akihojiwa na askari.  Gari lilivyokuwa kwa ndani baada ya kuwaka moto Askari wa Kikosi Maalum cha Zima Moto pamoja mashuhuda wa tukio hilo. MOROGORO:  Dereva wa gari dogo la mizigo aina ya lsuzu Carry (Kirikuu) lenye namba za usajiri T 609 CKW, amenusurika kifo baada ya gari hilo alilokuwa akiendesha kuwaka moto katika eneo la Masika katikati ya Mji wa Morogoro, leo Wakizungumza na mwanahabari wetu aliyefika eneo la tukio, mashuhuda wa tukio hilo Bernard Joseph na Juma ldd walisema; “Huyu dereva wa kirikuu alikuwa akitokea eneo la Msamvu (Kituo Kikuu cha Mabasi Yaendayo Mikoani) alipofika hapa Maska jirani na ‘round about’ tulishuhuida gari lake likiwaka moto kwa nyumba na yeye hakuwa na habari aliendelea na safari hivyo boda boda mmoja aliamua kuwasha pikipiki yake na kumkimbilia na kumjulisha tukio hilo ambapo alisimama na kushuhud

Heshima ya Samatta ndani ya KRC Genk inazidi kupanda kila kukicha

Image
Heshima ya mshambuliaji Mtanzania, Mbwana Samatta inazidi kupanda tartiiibu katika kikosi chake cha KRC Genk cha nchini Ubelgiji. Heshima ya Samatta imezidi kupanda kutokana na namna ambavyo amekuwa akifunga mfululizo. Kabla, haikuwa rahisi kuona Samatta akiwekwa kwenye matangazo ya kikosi hicho. Lakini sasa tayari ana mabao manne, hali inayomfanya Genk waone ni kati ya wachezaji wao muhimu. Katika matangazo mengi kuhusiana na mechi za Genk au mambo mengine muhimu, Samatta amekuwa akitumika, kitu ambacho awali ilikuwa aghalabu. Kutumika kwenye matangazo ni sehemu ya kuonyesha una mvuto au unakubalika. Jambo ambalo ni bora kwa Samatta na anachotakiwa ni kuongeza tu juhudi.

Wakala wa Yaya Toure amvaa Guardiol

Image
Wakala wa mchezaji Yaya Toure anaamini kwamba, ni kitendo Pep Guardiola kumwacha mchezaji huyo kwenye kikosi cha Ligi ya Mabingwa ni ukandamizaji wa wa hali ya juu, na kusisitiza kocha huyo atapswa kuomba radhi endapo atashindwa kuchukua kombe hilo. Toure, ambaye aliondoka Barcelona iilyokuwa chini ya Guardiola mwaka 2010 na kuhamia Man City, amebaki Etihad baada ya dirisha la usajili kufungwa rasmi na hivyo hana nafasi tena ya kushiriki Michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa. Mpaka sasa chini ya Guardiola, Toure amecheza mechi moja ya kuwania kufuzu kucheza makundi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Steaua Bucharest, hivyo wakala wake Dimitri Seluk. anaona ni wakati sahihi kwa mchezaji huyo kuondoka kwenye dirisha la usajili mwezi January. “Kama atachukua taji la Ligi ya Mabingwa msimu huu, basi nitasafiri mpaka England na nitasema mbele ya runinga kwamba Pep Guardiola ni meneja bora kabisa duniani,” Seluk alinukuliwa na gazeti la Sunday Mirror. “Lakini kama City hawatashinda Champions Leagu

Mbowe: Sidaiwi na NHC, Namiliki Jengo kwa Asilimia 75 Kuanzia Mwaka 1997

Image
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Mbowe amekana kudaiwa kiasi chochote na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akisema katika jengo hilo la Bilicanas la jijini Dar es Salaam, yeye si mpangaji bali ni mmiliki mwenza wa NHC. Alisema anamiliki jengo hilo kwa asilimia 75 tangu mwaka 1997 na kinachofanywa na shirika hilo la umma kinasimamiwa na viongozi wa dola kwa kuwa yeye ni mpinzani. “Mimi sidaiwi na NHC na madai yanayofanyika hayapo kisheria bali ni uharibifu wa makusudi unaolenga kunikomoa ambao unatokana na msimamo wangu kisiasa” alisema Mbowe. Alisema kuzongwazongwa huko ni kwa kuwa yeye ni mpinzani na kabla upinzani haujawa mkubwa alikuwa hafanyiwi hivyo. Kama ni kudaiwa, Serikali ina madeni, wafanyabiashara wana madeni lakini hawajafanyiwa kama anachofanyiwa Mbowe. Kwa nini Freemedia iwe ya kwanza kushambuliwa kwa kutoa kompyuta zake nje na kujaribu zake nje na kujaribu kuzikagua kwa ndani zina nini? Mbowe alihoji. Aliongeza kuwa si lazima