Posts

Nasri aonyesha hataki kurudi MAN City, aamua kuuza mjengo wake

Image
Nyota wa Man City, Samir Nasri ameamua kuliuza jumbo lake la kifahari la mjini Ceshire, England kwa kitita cha pauni million 5.7. Nasri ambaye sasa anakipiga kwa mkopo Sevilla ya Hispania ameamua kuliuza jumbo hilo lenye ukumbi wa disco, bwawa kubwa la kuogelea, stoo kubwa ya mvinyo na kadhalika. Uamuzi huo wa Nasri mwenye umri wa miaka 29 ni dalili ameamua kubaki Hispania na huenda akaishaiwishi Man City imuuze kabisa.

Bunduki 11 zakamatwa kwa mbunge

Image
Kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Serikali kupambana na tatizo sugu la ujangili, kimenasa bunduki 11 ambazo zinasadikiwa kutumika kufanya ujangili na kukamata watu wanne zaidi. Taarifa zilizopatikana jana zimelidokezea gazeti hili kuwa bunduki hizo zilikamatwa nyumbani kwa mbunge wa CCM (jina tunalihifadhi) ambaye bado anasakwa na kikosi kazi hicho. Matukio hayo yamekuja siku chache baada ya Rais John Magufuli kutaja jina la mtu anayeitwa Mpemba kuhusika na ujangili kwa muda mrefu wakati alipotembelea ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii na kushuhudia pembe 50 za ndovu zilizokamatwa na watumishi wa wizara hiyo. Siku hiyo, Rais aliwaambia watu aliowaita “vijana” waendelee na kazi yao ya kukamata wauaji wa tembo, akiwahakikishia kuwa Serikali ipo na kuwataka wasiogope mtu yeyote yule.

Azam nayo yaanza kulia na waamuzi Ligi Kuu Bara

Image
Kocha Mkuu wa Klabu ya Azam FC Zeben Hernandez amewataka waamuzi wa soka nchini kuchezesha mpira kwa kufuata sheria za soka ili kuboresha soka la Tanzania. Kocha Zeben amesema, changamoto kwa upande wa waamuzi imekuwa ikijirudia kila kukicha na siyo kwa sababu ya mchezo unaochezwa uwanjani, bali maamuzi yanaathiri klabu kama klabu, wachezaji wenyewe na hata makocha ambao wanakuwa wamejiandaa kwa ajili ya kupambana lakini mwisho wa siku waamuzi wanaharibu mchezo husika. Kauli ya Hernandez imekuja saa chache mara baada ya Azam FC kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar hapo usiku wa jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es salaam. Mtibwa Sugar ndiyo ilianza kuwa mbele kwenye mchezo huo baada ya kufunga bao la kushtukiza katika dakika ya pili likifungwa na Rashid Mandawa kabla ya nahodha wa Azam FC kwenye mchezo huo, Himid Mao, kusawazisha kwa mkwaju wa penalti kufuatia Henry Joseph, kuunawa mpira ndani ya eneo...

Pointi 3 kutoka Mbao FC zaendelea kuiweka Simba kileleni VPL

Image
 Goli pekee la Muzamiru Yassin dakika ya 86 limeipa Simba pointi tatu nyingine kwenye uwanja wa Uhuru jiji Dar es Salaam wakati wakipambana na timu iliyopanda ligi msimu huu Mbao FC kutoka jijini Mwanza.  Licha ya ugeni wao kwenye ligi, Mbao FC ambao wamepanda ligi kuu msimu kwa mara ya kwanza waliweza kuhimili vishindo vya wakongwe wa ligi hiyo Simba na kuchelewesha ushindi wao hadi dakika ya 86.  Blagnon ambaye aliingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya Laudit Mavugo, alitoa pasi ya goli kwa Mzamiru Yassin ambaye alikandamiza mpira nyavuni na kufunga bao lake la pili tangu ajiunge na Simba.  Mzamiru alifunga goli lake la kwanza ndani ya uzi wa Simba kwenye mechi iliyopita wakati Simba ilipocheza dhidi ya Kagera Sugar na kuifunga magoli 2-0 kwenye uwanja wa taifa.  Ushindi wa leo ni wa nane katika mechi 10 ambazo Simba wamecheza hadi sasa huku ukiwa ni ushindi wa tatu mfululizo wakiwa wametoka sare katika michezo miwili na kutopoteza mechi hata ...

AJALI: Basi la TARIKI lauwa Mtu 1 Lindi

Image
Bais la kampuni ya TARIKI linalo fanya safari zake Masasi Mtwara leo mida ya saa 6 mchana ilipofika maeneo ya Mnazi Mmoja Lindi Basi hilo lilipata Ajali Baada ya Dereva kushindwa kumudu Mwendo kasi na kupinduka, Ajali hiyo imesababisha Kifo cha Mtu mmoja...

Mapya yaibuka kipigo cha mwanafunzi Mbeya

Image
WAKATI  jamii ikiendelea kulaani kupigwa kikatili mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Kutwa ya Mbeya, Sebastian Chinguku, mwezi uliopita, imeelezwa kuwa wanafunzi wengi wamekosa nidhamu na wamejengewa kiburi na wazazi na walezi wao kudharau na kudhani wako juu ya walimu. Walimu wamesema pamoja na kwamba kitendo alichofanyiwa mwanafunzi Chinguku ni cha kikatili na kisichokubalika, lakini wengi wao hudhalilishwa na wanafunzi mbele ya wenzao, na wanapopewa adhabu, hutetewa na walezi na wazazi wao, jambo linalowaongezea kiburi na kutobadilika. Baadhi ya wazazi na walezi, wamekiri kutotekeleza ipasavyo wajibu wa kulea, ingawa wametupia lawama maendeleo ya teknolojia na makundi mabaya, kuchangia huwaharibu watoto wao huku wanafunzi wakieleza wazi kuwa nidhamu yao inahitaji kupigwa msasa. Walimu, wazazi na wanafunzi, kwa nyakati tofauti wakizungumza na gazeti hili, mara baada ya kutokea kwa tukio la Mbeya Day, walisema suala la maadili na miongozo ya adhabu pamoja na uhusiano kati ya ...

kuhakikisha inajenga Tanzania kuwa nchi ya viwanda

Image
Serikali imesisitiza kuwa Imejipanga kikamilifu  Serikali imesisitiza kuwa Imejipanga kikamilifu  kuhakikisha  inajenga Tanzania kuwa  nchi ya viwanda  kwa kutumia rasilimali zilizopo  bila kutegemea  misaada yenye masharti magumu  kutoka nje ya  nchi ili kuweza kufikia azma ya ajira kwa vijana. Hayo yamesemwa na  makamu wa rais Samia Suluhu Hassani wakati  akisalimiana na wakazi wa Morogoro Stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani  alipokuwa akielekea mjini  Dodoma kikazi , ambapo amesema vijana  wanatakiwa kujituma katika utendaji wa kazi  ili kuendana na kasi ya jitihada za serikali, kwani kuhusu ajira morogoro inatarajiwa kuwepo viwanda vya kutosha kuajiri vijana. Akizungumzia zoezi la upigaji chapa ya mifugo ambalo baadhi  ya  wafugaji waligoma kutekeleza zoezi hilo mkoani morogoro, amesisitiza wafugaji hao kutoa mifugo yao  ili iweze kutambuliwa kwa mujibu wa sheria ya mifugo  namba 12 ...