kuhakikisha inajenga Tanzania kuwa nchi ya viwanda
Serikali imesisitiza kuwa Imejipanga kikamilifu
Serikali imesisitiza kuwa Imejipanga kikamilifu kuhakikisha inajenga Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kutumia rasilimali zilizopo bila kutegemea misaada yenye masharti magumu kutoka nje ya nchi ili kuweza kufikia azma ya ajira kwa vijana.Hayo yamesemwa na makamu wa rais Samia Suluhu Hassani wakati akisalimiana na wakazi wa Morogoro Stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani alipokuwa akielekea mjini Dodoma kikazi , ambapo amesema vijana wanatakiwa kujituma katika utendaji wa kazi ili kuendana na kasi ya jitihada za serikali, kwani kuhusu ajira morogoro inatarajiwa kuwepo viwanda vya kutosha kuajiri vijana.
Akizungumzia zoezi la upigaji chapa ya mifugo ambalo baadhi ya wafugaji waligoma kutekeleza zoezi hilo mkoani morogoro, amesisitiza wafugaji hao kutoa mifugo yao ili iweze kutambuliwa kwa mujibu wa sheria ya mifugo namba 12 ya mwaka 2012. Aidha zoezi hilo litasaidia kutambua mifugo inayoingizwa ndani na nje nchi kinyemela.
Comments
Post a Comment