Pointi 3 kutoka Mbao FC zaendelea kuiweka Simba kileleni VPL


 Goli pekee la Muzamiru Yassin dakika ya 86 limeipa Simba pointi tatu nyingine kwenye uwanja wa Uhuru jiji Dar es Salaam wakati wakipambana na timu iliyopanda ligi msimu huu Mbao FC kutoka jijini Mwanza.

 Licha ya ugeni wao kwenye ligi, Mbao FC ambao wamepanda ligi kuu msimu kwa mara ya kwanza waliweza kuhimili vishindo vya wakongwe wa ligi hiyo Simba na kuchelewesha ushindi wao hadi dakika ya 86.

 Blagnon ambaye aliingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya Laudit Mavugo, alitoa pasi ya goli kwa Mzamiru Yassin ambaye alikandamiza mpira nyavuni na kufunga bao lake la pili tangu ajiunge na Simba.

 Mzamiru alifunga goli lake la kwanza ndani ya uzi wa Simba kwenye mechi iliyopita wakati Simba ilipocheza dhidi ya Kagera Sugar na kuifunga magoli 2-0 kwenye uwanja wa taifa.

 Ushindi wa leo ni wa nane katika mechi 10 ambazo Simba wamecheza hadi sasa huku ukiwa ni ushindi wa tatu mfululizo wakiwa wametoka sare katika michezo miwili na kutopoteza mechi hata moja. (Simba 3-1 Ndanda FC, JKT Ruvu 0-0 Simba, Simba 2-1 Ruvu Shooting, Simba 2-0 Mtibwa Sugar, Azam 0-1 Simba, Simba 4-0 Majimaji, Yanga 1-1 Simba, Mbeya City 0-2 Simba, Simba 2-0 Kagera Sugar na Simba 1-0 Mbao FC).

 Mchezo ujao wa Simba utakuwa dhidi ya Toto African ya Mwanza mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Uhuru wakati Mbao wao watakuwa uwanja wa Sokoine kukabiliana na Tanzania Prisons.

Comments

Popular posts from this blog

UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI

YANGA YAPATA PIGO, KIPA WAKE NAMBA MOJA DEO MUNISHI AFIWA NA BABA YAKE

Kwa Nini Watu Wengi Wanaamini Uchawi Unaleta Mafanikio?