Posts

Showing posts from 2016

690 mbaroni kwa uhalifu wa mtandao

Image
SERIKALI kupitia kitengo maalum cha uchunguzi wa jinai ya kimtandao, imefanikiwa kukamata watuhumiwa 690 kwa tuhuma za kufanya uhalifu wa mtandao. Watuhumiwa hao ni matapeli, wezi, waporaji wa simu za mkononi na wengineo wanaotumia mfumo wa intaneti kuibia watu wasiokuwa na hatia. Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Projestus Rwegasira alisema juzi jioni kuwa ofisi yake imekuwa ikikabiliana kikamilifu na wahalifu hao. Alisitiza kwamba wahusika wote wa vitendo hivyo, watakamatwa. Meja Jenerali Rwegasira alikuwa akizungumza katika mahojiano katika kipindi cha Tunatekeleza, kinachorushwa na Televisheni ya Taifa(TBC). Kwamba wizara yake kwa kushirikiana na vyombo vya serikali, inaandaa mashtaka dhidi ya watuhumiwa waliokamatwa na watafikishwa mahakamani. “Tunafanya kila juhudi kuzuia vitendo vya uhalifu wa kimtandao, tayari tumekamata baadhi ya watuhumiwa na watakabiliana na mkono wa sheria mahakamani,” alisema. Alisema serikali imeunda kitengo maalumu chini ya Wiz

Tanzania yapaa kiuchumi kusini mwa Jangwa la Sahara

Image
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema Tanzania imebaki kuwa miongoni mwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara Barani Afrika, ambazo uchumi wake unakua kwa kasi. Dk Mpango alisema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya uchumi wa taifa kwa kipindi cha Julai hadi Desemba, 2016 na matarajio hadi Juni, 2017. Alisema ukuaji wa uchumi ni mojawapo ya vitu vinavyotazamwa katika kutathmini afya ya uchumi wa taifa. Akifafanua, alitoa mfano kwa baadhi ya nchi hizo kuwa mwaka jana Tanzania uchumi wake ulikuwa kwa asilimia 7.0 na mwaka huu unakua asilimia 7.2, Kenya mwaka jana ulikua asilimia 5.6 na mwaka huu unakua asilimia 6.0, Uganda mwaka jana ulikuwa asilimia 4.8 na mwaka huu unakuwa asilimia 4.9. “Kwa mifano hiyo tunaona Tanzania imeendelea kufanya vizuri uchumi unakuwa kwa kasi kubwa katika Bara la Afrika,” alisema. Kwa upande mwingine, alisema kuwa ustawi wa uchumi wa taifa unapimwa kwa kuangalia viashiria mbalimbali vi

13,626 wanaswa Dar kwa ujambazi, ‘unga’

Image
KIKOSI cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imekamata jumla ya watuhumiwa 13,626 na kuwafikishwa mahakamani kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo dawa za kulevya na ujambazi wa kutumia silaha kwa kipindi cha mwaka mmoja wa 2016. Aidha, hali ya uhalifu wa kutumia silaha katika jiji la Dar es Salaam umepungua, ukilinganisha na mwaka uliopita wa 2015 na matukio yanayoongezeka kwa wingi ni ya ubakaji na ulawiti. Akitoa tathmini ya mwaka mmoja, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha yamepungua kutoka 204 mwaka jana hadi 127 mwaka huu. Idadi hiyo ni pungufu ya matukio 77, sawa na asilimia 37.7 huku matukio ya kutumia nguvu yamepungua kutoka 1,181 mwaka jana hadi 874 sawa na asilimia 26. Kamishna Sirro alifafanua kuwa matukio ya mauaji, yamepungua kwa asilimia 11 ukilinganisha na mwaka jana, ambapo kulikuwa na jumla ya matukio 327 wakati kwa mwaka huu ni matukio 291 pungufu ya matukio 36. Alisema matukio ya

Nasri aonyesha hataki kurudi MAN City, aamua kuuza mjengo wake

Image
Nyota wa Man City, Samir Nasri ameamua kuliuza jumbo lake la kifahari la mjini Ceshire, England kwa kitita cha pauni million 5.7. Nasri ambaye sasa anakipiga kwa mkopo Sevilla ya Hispania ameamua kuliuza jumbo hilo lenye ukumbi wa disco, bwawa kubwa la kuogelea, stoo kubwa ya mvinyo na kadhalika. Uamuzi huo wa Nasri mwenye umri wa miaka 29 ni dalili ameamua kubaki Hispania na huenda akaishaiwishi Man City imuuze kabisa.

Bunduki 11 zakamatwa kwa mbunge

Image
Kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Serikali kupambana na tatizo sugu la ujangili, kimenasa bunduki 11 ambazo zinasadikiwa kutumika kufanya ujangili na kukamata watu wanne zaidi. Taarifa zilizopatikana jana zimelidokezea gazeti hili kuwa bunduki hizo zilikamatwa nyumbani kwa mbunge wa CCM (jina tunalihifadhi) ambaye bado anasakwa na kikosi kazi hicho. Matukio hayo yamekuja siku chache baada ya Rais John Magufuli kutaja jina la mtu anayeitwa Mpemba kuhusika na ujangili kwa muda mrefu wakati alipotembelea ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii na kushuhudia pembe 50 za ndovu zilizokamatwa na watumishi wa wizara hiyo. Siku hiyo, Rais aliwaambia watu aliowaita “vijana” waendelee na kazi yao ya kukamata wauaji wa tembo, akiwahakikishia kuwa Serikali ipo na kuwataka wasiogope mtu yeyote yule.

Azam nayo yaanza kulia na waamuzi Ligi Kuu Bara

Image
Kocha Mkuu wa Klabu ya Azam FC Zeben Hernandez amewataka waamuzi wa soka nchini kuchezesha mpira kwa kufuata sheria za soka ili kuboresha soka la Tanzania. Kocha Zeben amesema, changamoto kwa upande wa waamuzi imekuwa ikijirudia kila kukicha na siyo kwa sababu ya mchezo unaochezwa uwanjani, bali maamuzi yanaathiri klabu kama klabu, wachezaji wenyewe na hata makocha ambao wanakuwa wamejiandaa kwa ajili ya kupambana lakini mwisho wa siku waamuzi wanaharibu mchezo husika. Kauli ya Hernandez imekuja saa chache mara baada ya Azam FC kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar hapo usiku wa jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es salaam. Mtibwa Sugar ndiyo ilianza kuwa mbele kwenye mchezo huo baada ya kufunga bao la kushtukiza katika dakika ya pili likifungwa na Rashid Mandawa kabla ya nahodha wa Azam FC kwenye mchezo huo, Himid Mao, kusawazisha kwa mkwaju wa penalti kufuatia Henry Joseph, kuunawa mpira ndani ya eneo

Pointi 3 kutoka Mbao FC zaendelea kuiweka Simba kileleni VPL

Image
 Goli pekee la Muzamiru Yassin dakika ya 86 limeipa Simba pointi tatu nyingine kwenye uwanja wa Uhuru jiji Dar es Salaam wakati wakipambana na timu iliyopanda ligi msimu huu Mbao FC kutoka jijini Mwanza.  Licha ya ugeni wao kwenye ligi, Mbao FC ambao wamepanda ligi kuu msimu kwa mara ya kwanza waliweza kuhimili vishindo vya wakongwe wa ligi hiyo Simba na kuchelewesha ushindi wao hadi dakika ya 86.  Blagnon ambaye aliingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya Laudit Mavugo, alitoa pasi ya goli kwa Mzamiru Yassin ambaye alikandamiza mpira nyavuni na kufunga bao lake la pili tangu ajiunge na Simba.  Mzamiru alifunga goli lake la kwanza ndani ya uzi wa Simba kwenye mechi iliyopita wakati Simba ilipocheza dhidi ya Kagera Sugar na kuifunga magoli 2-0 kwenye uwanja wa taifa.  Ushindi wa leo ni wa nane katika mechi 10 ambazo Simba wamecheza hadi sasa huku ukiwa ni ushindi wa tatu mfululizo wakiwa wametoka sare katika michezo miwili na kutopoteza mechi hata moja. (Simba 3-1 Ndanda

AJALI: Basi la TARIKI lauwa Mtu 1 Lindi

Image
Bais la kampuni ya TARIKI linalo fanya safari zake Masasi Mtwara leo mida ya saa 6 mchana ilipofika maeneo ya Mnazi Mmoja Lindi Basi hilo lilipata Ajali Baada ya Dereva kushindwa kumudu Mwendo kasi na kupinduka, Ajali hiyo imesababisha Kifo cha Mtu mmoja...

Mapya yaibuka kipigo cha mwanafunzi Mbeya

Image
WAKATI  jamii ikiendelea kulaani kupigwa kikatili mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Kutwa ya Mbeya, Sebastian Chinguku, mwezi uliopita, imeelezwa kuwa wanafunzi wengi wamekosa nidhamu na wamejengewa kiburi na wazazi na walezi wao kudharau na kudhani wako juu ya walimu. Walimu wamesema pamoja na kwamba kitendo alichofanyiwa mwanafunzi Chinguku ni cha kikatili na kisichokubalika, lakini wengi wao hudhalilishwa na wanafunzi mbele ya wenzao, na wanapopewa adhabu, hutetewa na walezi na wazazi wao, jambo linalowaongezea kiburi na kutobadilika. Baadhi ya wazazi na walezi, wamekiri kutotekeleza ipasavyo wajibu wa kulea, ingawa wametupia lawama maendeleo ya teknolojia na makundi mabaya, kuchangia huwaharibu watoto wao huku wanafunzi wakieleza wazi kuwa nidhamu yao inahitaji kupigwa msasa. Walimu, wazazi na wanafunzi, kwa nyakati tofauti wakizungumza na gazeti hili, mara baada ya kutokea kwa tukio la Mbeya Day, walisema suala la maadili na miongozo ya adhabu pamoja na uhusiano kati ya mwan

kuhakikisha inajenga Tanzania kuwa nchi ya viwanda

Image
Serikali imesisitiza kuwa Imejipanga kikamilifu  Serikali imesisitiza kuwa Imejipanga kikamilifu  kuhakikisha  inajenga Tanzania kuwa  nchi ya viwanda  kwa kutumia rasilimali zilizopo  bila kutegemea  misaada yenye masharti magumu  kutoka nje ya  nchi ili kuweza kufikia azma ya ajira kwa vijana. Hayo yamesemwa na  makamu wa rais Samia Suluhu Hassani wakati  akisalimiana na wakazi wa Morogoro Stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani  alipokuwa akielekea mjini  Dodoma kikazi , ambapo amesema vijana  wanatakiwa kujituma katika utendaji wa kazi  ili kuendana na kasi ya jitihada za serikali, kwani kuhusu ajira morogoro inatarajiwa kuwepo viwanda vya kutosha kuajiri vijana. Akizungumzia zoezi la upigaji chapa ya mifugo ambalo baadhi  ya  wafugaji waligoma kutekeleza zoezi hilo mkoani morogoro, amesisitiza wafugaji hao kutoa mifugo yao  ili iweze kutambuliwa kwa mujibu wa sheria ya mifugo  namba 12 ya mwaka 2012. Aidha zoezi hilo  litasaidia kutambua mifugo inayoingizwa ndani na nje nchi  ki

Jinsi ya kupata ngozi laini

Image
Takribani kila mtu angependa kuwa na ngozi laini, au hata laini zaidi. Watu wengi wamekuwa wakiitafuta ngozi nzuri au kujitahidi kuitunza ili isiharibike. Lakini je, wamefanikiwa? Wachache hufanikiwa na wengi hushindwa. Na hata hao waliofanikiwa wengi wao hutumia vipodozi vikali ambavyo vingi huchubua na kuharibu ngozi zao na kuwaletea madhara makubwa sana baadae. Vipi wewe, ungependa kuwa na ngozi nzuri bila kuidhuru afya yako? Karibu somo la leo ili uweze kuwa na ngozi nzuri bila kuidhuru afya yako. Ngozi laini ni nzuri na inaongeza mvuto wa mwili. Ulaini wa ngozi hupotezwa na mambo mbalimbali kama vile seli za ngozi kupungukiwa na maji na kuanza kusinyaa na kunyauka, seli za ngozi kujeruhiwa,  na seli za ngozi kufa. Matokeo yake ni michirizi, makunyanzi, makovu, chunusi, madoa, ngozi kufubaa na kuzeeka. Kuifanya ngozi kuwa laini unahitaji kuupatia mwili virutubisho vyote vya kujenga mwili vizuri na kunywa maji ya kutosha ili seli zisikauke, kusinyaa wala kunyauka. Kula mlo kami

Simba yaipa kichapo Kagera Suger 2 - 0 uwanja wa Uhuru jijini Dar leo

Image
Simba imezidi kujichimbia kileleni baada ya kuichapa Kagera Sugar kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Simba iemfikisha pointi 23 kileleni baada ya ushindi huo wa mabao yake yaliyofungwa na Muzamiru Yasini na Shiza Kichuya. MECHI NYINGINE LEO: JKT Ruvu 1-1 Mwadui Stand United 1-1 African Lyon

Arsenal washinda, Man City sare na Everton

Image
 Mabingwa watetezi wa Lig ya Premia Leicester City wamecharazwa 3-0 na Chelsea uwanjani Stamford Bridge nao Arsenal wakafanikiwa kuondoka na ushindi dhidi ya Swansea City licha ya kusalia na wachezaji 10 uwanjani. Mabao ya Chelsea yalifungwa na Diego Costa, Eden Hazard na Victor Moses. Theo Walcott alifunga mawili upande wa Arsenal kabla ya Gylfi Sigurdsson kukomboa moja upande wa Swansea. Mesut Ozil aliwarejesha Arsenal mabao mawili mbele baada ya kufikia krosi ya kabla ya nguvu mpya Borja Baston kufunga la pili upande wa Swansea. Granit Xhaka wa Arsenal alioneshwa kadi nyekundu lakini wakafanikiwa kukwamilia ushindi wao. Uwanjani Etihad, vijana wa Pep Guardiola wametoka sare 1-1 na Everton. Everton walitangulia kufunga kupitia Romelu Lukaku. City walikomboa kupitia Nolito. Mechi iliyoshangaza wengi ni ya Bournemouth ambao wamepata ushindi mkubwa wa 6-1 dhidi ya Hull City. Matokeo kamili ya mechi za leo Arsenal 3-2 Swansea Bournemouth 6-1 Hull Man City 1-1 Everton Stoke 2-

Mkuu wa mkoa wa Mwanza amezindua meli kubwa ya kisasa yenye uwezo wa kubeba abiria 500.

Image
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela amezindua rasmi huduma ya usafiri wa meli kati ya Mwanza na mji wa Nansio wilayani Ukerewe katika ziwa Victoria, ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 500 magari madogo 40 na tani 284 za mizigo, hatua itakayosaidia kutatua changamoto ya huduma za usafiri wa abiria kwa wakazi wa kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza. Meli hiyo MV. Nyehunge II, imejengwa na kampuni ya Songoro Marine Transport kwa gharama ya shilingi milioni 800 na kufanyiwa ukaguzi na maofisa wa mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMTRA), makao makuu Dar es Slaam. Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Ukerewe, akiwemo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo George Nyamaha wanaeleza changamoto za usafiri zilizokuwa zinawakabili awali. Meli zinazotoa huduma ya usafiri ndani ya ziwa Victoria kati ya Mwanza na Ukerewe, ni mv. Butiama inayomilikiwa na kampuni ya huduma za meli Tanzania pamoja na meli ya MV. Nyehunge.

Dalili Ya Ng'ombe Mwenye Afya

Image
 Ng'ombe mwenye afya kwa kawaida pua yake huwa na unyevu unyevu au kama vile inatoa jasho jembamba sana.Ukiona ng'ombe wako ana pua iliyokauka na haina unyevuunyevu basi ujue hiyo ni dalili kwamba kuna tatizo katika mwili wake, hii inaweza pia kuwa dalili ya maambukizi au magonjwa  Pua ya ng'ombe inauwezo wa kunusa umbali wa kilometa 8 au maili 5, ndio maana wanaweza kukimbia machungoni au hata kuvunja banda na kufuata mazao mashambani sababu ya harufu, msimu wa membe tatizo la kutoroka ndio huwa kubwa hasa maembe yapaoanza kuiva Kwa siku hutumia masaa 6 kula chakula na hutumia masaa 8 kucheua na na kutafuna tena na hunywa maji kiasi cha lita 12 mpaka 25 kutegemeana na ukubwa na hula kiasi cha kilo mpaka 45 kwa ng'ombe wakubwa Ng'ombe mwenye kilo 1000 huweza kuzalisha kiasi cha tani 10 za mbolea kwa mwaka Ng'ombe aina ya friesian (pichani juu)ambao ni kinara wa uzalishaji wa maziwa duniani wana rangi nyeupa na mabaka meusi ambapo haya mabaka

Picha: Vijana 30 kutoka nchi 5 waingia kwenye kijiji cha Maisha Plus

Image
Masoud na Babu wa Kijijini wakiteta jambo  Vijana 30 kutoka nchi tano za Afrika Mashariki, Jumapili hii waliingia rasmi kwenye kijiji cha shindano la Maisha Plus. Kuwasili kwa vijana hao katika kijiji hicho ambacho hakijulikani kilipo, kulikuwa kukirushwa live kupitia kituo cha runinga cha Azam Two. Wakiwa na mabegi yao mkononi, washiriki hao walipokelewa na mwanzilishi wa kipindi hicho, Masoud Kipanya huku wakiwa wamefunikiwa vitambaa vyeusi machoni. Babu akikagua himaya yake Mshindi wa shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 30. Washiriki wote watapewa shilingi 7,000 kwa wiki ili kujikimu wakiwa kwenye kijiji hicho kilichopo katikati ya msitu. Lengo la kupewa shilingi 1,000 kila siku ni kuwafunza maisha ya waafrika wengi ambao huishi chini ya dola moja kwa siku. Hakuna nyumba kwenye kijiji hicho na hivyo watatakiwa kujenga nyumba zao wenyewe za kuishi. Tazama picha zaidi hapo chini.  Washiriki wakiwa wamefunikwa vitambaa vyeusi usoni mwao  Babu akim