Posts

Orodha mauaji dada’ke Bilionia Msuya yaongezeka

Image
Marehemu Aneth Msuya .  Dar es Salaam.  Idadi ya washtakiwa katika kesi ya mauaji ya Aneth Msuya ambaye alikuwa dada wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Erasto Msuya maarufu bilionea Msuya, imeongezeka na kufikia wawili baada ya mwingine kuunganishwa nayo. Awali, Agosti 23, mwaka huu mshtakiwa Miriam Mrita (41) ambaye ni mke wa bilionea huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth aliyekuwa wifi yake. Hata hivyo, juma moja baadaye, mfanyabiashara wa jijini Arusha, Revocatus Evarist (40),  alipandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo na kuuunganishwa na Miriam kwenye kesi hiyo. Evarist alipandishwa kizimbani mahakamani hapo Ijumaa iliyopita na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo.

Picha 10: Dereva wa Kirikuu Anusurika Kifo Baada ya Gari Lake Kuwaka Moto

Image
 Gari lilivyowaka.  Mashuhuda  Mashuhuda.  Dereva wa gari hilo, Michael Augustino akitoa taarifa kwa bosi wake.  Michael akihojiwa na askari.  Gari lilivyokuwa kwa ndani baada ya kuwaka moto Askari wa Kikosi Maalum cha Zima Moto pamoja mashuhuda wa tukio hilo. MOROGORO:  Dereva wa gari dogo la mizigo aina ya lsuzu Carry (Kirikuu) lenye namba za usajiri T 609 CKW, amenusurika kifo baada ya gari hilo alilokuwa akiendesha kuwaka moto katika eneo la Masika katikati ya Mji wa Morogoro, leo Wakizungumza na mwanahabari wetu aliyefika eneo la tukio, mashuhuda wa tukio hilo Bernard Joseph na Juma ldd walisema; “Huyu dereva wa kirikuu alikuwa akitokea eneo la Msamvu (Kituo Kikuu cha Mabasi Yaendayo Mikoani) alipofika hapa Maska jirani na ‘round about’ tulishuhuida gari lake likiwaka moto kwa nyumba na yeye hakuwa na habari aliendelea na safari hivyo boda boda mmoja aliamua kuwasha pikipiki yake na kumkimbilia na kumjulisha tukio...

Heshima ya Samatta ndani ya KRC Genk inazidi kupanda kila kukicha

Image
Heshima ya mshambuliaji Mtanzania, Mbwana Samatta inazidi kupanda tartiiibu katika kikosi chake cha KRC Genk cha nchini Ubelgiji. Heshima ya Samatta imezidi kupanda kutokana na namna ambavyo amekuwa akifunga mfululizo. Kabla, haikuwa rahisi kuona Samatta akiwekwa kwenye matangazo ya kikosi hicho. Lakini sasa tayari ana mabao manne, hali inayomfanya Genk waone ni kati ya wachezaji wao muhimu. Katika matangazo mengi kuhusiana na mechi za Genk au mambo mengine muhimu, Samatta amekuwa akitumika, kitu ambacho awali ilikuwa aghalabu. Kutumika kwenye matangazo ni sehemu ya kuonyesha una mvuto au unakubalika. Jambo ambalo ni bora kwa Samatta na anachotakiwa ni kuongeza tu juhudi.

Wakala wa Yaya Toure amvaa Guardiol

Image
Wakala wa mchezaji Yaya Toure anaamini kwamba, ni kitendo Pep Guardiola kumwacha mchezaji huyo kwenye kikosi cha Ligi ya Mabingwa ni ukandamizaji wa wa hali ya juu, na kusisitiza kocha huyo atapswa kuomba radhi endapo atashindwa kuchukua kombe hilo. Toure, ambaye aliondoka Barcelona iilyokuwa chini ya Guardiola mwaka 2010 na kuhamia Man City, amebaki Etihad baada ya dirisha la usajili kufungwa rasmi na hivyo hana nafasi tena ya kushiriki Michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa. Mpaka sasa chini ya Guardiola, Toure amecheza mechi moja ya kuwania kufuzu kucheza makundi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Steaua Bucharest, hivyo wakala wake Dimitri Seluk. anaona ni wakati sahihi kwa mchezaji huyo kuondoka kwenye dirisha la usajili mwezi January. “Kama atachukua taji la Ligi ya Mabingwa msimu huu, basi nitasafiri mpaka England na nitasema mbele ya runinga kwamba Pep Guardiola ni meneja bora kabisa duniani,” Seluk alinukuliwa na gazeti la Sunday Mirror. “Lakini kama City hawatashinda Champions Leagu...

Mbowe: Sidaiwi na NHC, Namiliki Jengo kwa Asilimia 75 Kuanzia Mwaka 1997

Image
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Mbowe amekana kudaiwa kiasi chochote na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akisema katika jengo hilo la Bilicanas la jijini Dar es Salaam, yeye si mpangaji bali ni mmiliki mwenza wa NHC. Alisema anamiliki jengo hilo kwa asilimia 75 tangu mwaka 1997 na kinachofanywa na shirika hilo la umma kinasimamiwa na viongozi wa dola kwa kuwa yeye ni mpinzani. “Mimi sidaiwi na NHC na madai yanayofanyika hayapo kisheria bali ni uharibifu wa makusudi unaolenga kunikomoa ambao unatokana na msimamo wangu kisiasa” alisema Mbowe. Alisema kuzongwazongwa huko ni kwa kuwa yeye ni mpinzani na kabla upinzani haujawa mkubwa alikuwa hafanyiwi hivyo. Kama ni kudaiwa, Serikali ina madeni, wafanyabiashara wana madeni lakini hawajafanyiwa kama anachofanyiwa Mbowe. Kwa nini Freemedia iwe ya kwanza kushambuliwa kwa kutoa kompyuta zake nje na kujaribu zake nje na kujaribu kuzikagua kwa ndani zina nini? Mbowe alihoji. Aliongeza kuwa si la...

Sh225 mil zahudumiwa wanafunzi hewa

Image
Kahama.  Wanafunzi hewa waliobainika wilayani Kahama, wameisababishia hasara Serikali ya Sh225 milioni kwa kipindi cha miezi minane kuanzia Januari hadi Agosti. Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkulu alisema kamati maalumu aliyounda imebaini uwapo wa wanafunzi hewa 29,000, ambao wamekuwa wakiisababishia hasara Serikali kila mwezi. “Serikali ya Awamu ya Tano tangu iingie madarakani imekuwa ikituma fedha kila shule kwenye mpango wa elimu bure, lakini maofisa elimu, waratibu kata, walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari wamebuni mbinu za kula fedha hizo kwa kuweka wanafunzi hewa kwenye shule zao,” alisema Nkulu. Alitoa siku tatu kwa kila halmashauri kuwasilisha takwimu sahihi za wanafunzi ambazo zitalingana na idadi aliyonayo iliyopatikana baada ya kamati ya uchunguzi.

Baada ya Ngasa kuvunja mkataba South, Kocha wa Yanga atoa kauli hii

Image
 Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amempa ugumu aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Free States ya Afrika Kusini, Mrisho Ngassa kurejea kuichezea timu hiyo. Hiyo, ni siku moja tangu taarifa za kiungo huyo kusitisha mkataba wake wa kuichezea Free States kwa makubaliano huku tetesi zikienea kuwa nyota huyo atarejea kucheza Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo la Ligi Kuu Bara msimu huu. Ngassa, alisitisha mkataba wa kuendelea kukipiga Sauz kwa kile alichodai kuwa timu hiyo haina malengo ya kutwaa ubingwa zaidi kushiriki kwenye ligi kuu. Pluijm alisema kwenye kikosi chake hahitaji kiungo mshambuliaji kwani tayari anao wanne, tena vijana wenye uwezo mkubwa wa kuendana na kasi yake. Pluijm aliwataja viungo hao washambuliaji kuwa ni Mzambia, Obrey Chirwa, Juma Mahadhi, Simon Msuva na Deus Kaseke ambao anaamini bado wana uwezo mkubwa wa kuichezea timu hiyo kwa muda mrefu kutokana na umri wao. Aliongeza kuwa, haoni sababu ya kujaza viungo wengi washambuliaji kwenye kikosi cha...