Hatimaye Shamsa Ford Afunga Ndoa na Chidi Mapenzi



 STAA wa Bongo filamu nchini, Shamsa Ford amefunga ndoa na Rashidi Said ‘Chidi Mapenzi’ ambaye ni mfanyabiashara wa maduka ya nguo.

Sherehe za ndoa hiyo zilifanyika nyumbani kwa wazazi wa Shamsa eneo la Sinza, Afrikasana jijini Dar es Salaam.

 Awali, Shamsa alidumu katika penzi na Dickson Matoke ‘Dick’ na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Terry na kisha  kufunga ndoa ya kimila nyumbani kwa mwanaume huyo, Tarime mkoani Mara ila baadaye waliachana na kuangukia kwa staa wa Bongo Fleva Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’  ambaye penzi lao halikudumu.





Comments

Popular posts from this blog

Alichokisema aliyekuwa katibu wa chadema mkoani Mwanza baada ya kutimkia CCM

Mkuu wa mkoa wa Mwanza amezindua meli kubwa ya kisasa yenye uwezo wa kubeba abiria 500.

UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI