Posts

Taarifa kwa Umma kuaribika kwa mashine ya MRI hospitali ya taifa Muhimbili

Image
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inapenda kuujulisha umma kwamba mashine ya MRI itasimama kwa muda kufanya kazi baada ya kuharibiika. Mashine hii iliharibiika tarehe 24/08/2016 baada ya kutokea hitilafu ya umeme. Baada ya kuharibiika, tarehe hiyo (24/08/2016) mafundi wa Philips kwa kushirikiana na mafundi wetu walianza kutafuta athari baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme. Tarehe 26/08/2016, mafundi walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika mashine hii kwa kuwa betri za awali zilikuwa zimefungwa muda mrefu. Tarehe 28/08/2016 mafundi walibaini kwamba kifaa cha Gradient Module kilikuwa kimeharibiika na tayari hospitali kwa kushirikiana na Philips wameagiza kifaa hicho kutoka Uholanzi. Hospitali ya Taifa Muhimbili inawaomba radhi wananchi kwa usumbufu wowote uliojitokeza. Imetolewa na;                                                 ...

Aliyedaiwa kufariki Dunia miaka 200 iliyopita, apatikana hai

Image
Binadamu  anaesadikiwa kufariki zaidi ya miaka 200 iliyopita amepatikana akiwa hai nchini Mongolia katika hali ya kutojiweza au kupooza. Mzimu huo uliopatikana katika mji wa Songino Khairkhan nchini Mongolia, ulivumbuliwa na mtu aliejulikana kama Dalai Rama na unasadikiwa kuishi miaka ya zamani sana maeneo ya China na India. Dk Barry Kerzin ndiye alieufanyia uchunguzi mwili huo na kuthibitisha kuwa binadamu huyo aliishi mnamo karne ya nne au ya sita kabla ya kuzaliwa kristo na tangu alipofariki ni zaidi ya miaka 200 imepita. Wananchi wa eneo hilo wanaamini jambo hilo lina imani za kishirikina ndani yake na wengine wakidai mizimu hiyo huonekana mara kwa mara nchini India.

Asamoah Gyan arudi Uingereza

Image
Nahodha wa kikosi cha soka nchini Ghana Asamoah Gyan anatarajiwa kujiunga na klabu ya Reading kwa mkopo kutoka timu ya China Shanghai SIPG. Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Sunderland anafanyiwa ukaguzi wa matibabu na klabu hiyo ya daraja la kwanza. Gyan aliifungia mabao 30 Sunderland alipoichezea timu hiyo kwa misimu miwili,kutoka mwaka 2010 kabla ya kuelekea Al-Ain ya Umoja wa Milki za kiarabu UAE. Alijiunga na Shanghai 2015 wakati huo na alikuwa miongoni mwa mchezaji wanaolipwa zaidi duniani.

Lowassa, Mbowe, Mnyika wakamatwa

Image
Dar es Salaam.  Viongozi wa Chadema wamekamatwa na polisi na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano. Akizungumzia kukamatwa kwa viongozi hao Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema waliokamatwa na polisi kwa ajili ya mahojiano ni Edward Lowassa, Freeman Mbowe, John Mnyika, Dk Vincent Mashinji na  Said Issah                        “Tulikuwa kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichojumuisha wajumbe na wabunge kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya chama. Jumla ya wajumbe walikuwa 170. Tukiwa kwenye kiako walikuja watu wanasema tunatakiwa polisi kwa sababu tumekiuka agizo la lilitokataza mikutano.”

Daladala lagonga magari matatu maji matitu Temeke jijini Dar es Salaam

Image
  Wananchi wakiangalia ajali iliyosababishwa na daladala lenye namba za usajili T 397 BVB linalofanya safari zake kati ya Temeke na Gongo la Mboto kwa kuyagonga magari mengine matatu eneo la Maji Matitu Temeke Dar es Salaam leo asubuhi. Katika ajali hiyo dereva wa gari dogo namba T 628 DFE alijeruhiwa.   Gari dogo namba T 628 DFE lililogongwa na daladala hilo likiwa limeharibika.   Daladala hiloegonga gari namba T 458 CAN.   Askari wa Usalama barabarani akiangalia ajali hiyo. Daladala uso kwa uso na gari dogo. MKAZI  wa Chamazi ambaye ni mwanamke amejeruhiwa baada ya gari lake dogo alilokuwa akiendesha kugongwa na daladala lenye namba T 397 BVB linadodaiwa kuiba njia. Ajali hiyo imetokea Maji Matitu Temeke jijini Dar es Salaam leo  asubuhi ambapo daladala hilo pia liliyagonga magari mengine matatu na kuzua kizaazaa katika barabara ya Charambe kwenda Chamazi. Mkazi wa eneo hilo Hamisi Juma aliyeshuhudia ajali hiyo amesema ...

Mchezaji avunjiwa mkataba baada ya kugundulika ana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU)

Image
 Zikiwa zimepita siku nne tu tangu asajiliwe na klabu ya Al Ittihad inayoshiki ligi kuu ya Misri, Samuel Nlend, 21, mkataba wake umevunjwa baada ya klabu yake mpya kugundua mchezaji huyo anamaambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU). Jarid linalojulikana kwa jina la KingFut.com limeripoti kuwa, afisa habari wa klabu hiyo amethibitisha taarifa hiyo ya kusikitisha kwa vyombo vya habari. Mshambuliaji huyo ameitumikia Cameroon katika michezo mitano, alifunga goli January kwenye michuano ya mataifa ya Afrika kabla ya kujiunga na Al Ittihad majira ya kiangazi.  Samuel Nlend alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Al Ittihad tangu tarehe 24 August. Licha ya hayo yote kutokea bado amepata support ya kutosha kutoka kwa klabu yake mpya ya Misri.

Maelfu ya watu waokolewa pwani ya Libya

Image
 Meli za wanamaji wa Uhispania na Italia zimewaokoa maelfu ya watu nje ya pwani ya Libya hii leo. Takriban watu 3000 waliokolewa mapema leo kutoka zaii ya mashua 20 za mbao. Licha ya watu wengi kushangilia wakati meli za uokoaji zilipowasili na kuruka kupiga mbizi kuelekea kwa meli hizo, wengine walisalia kuwangalia watoto wao. Shirika la habari la AP linasema kuwa idadi kubwa ya watu hao ni kutoa nchini Eritrea.