Posts

Showing posts from January, 2017

TRA yanasa mali za mabilioni Dar

Image
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata bidhaa za magendo, zilizoingizwa nchini kwa njia ya panya, ambazo zimeipotezea serikali kodi ya Sh bilioni 3.3 huku zikiwa na thamani ya jumla ya Sh bilioni 4. Aidha, imetaja maeneo korofi yanayotumika kuingiza bidhaa hizo kuwa ni Bagamoyo, Saadani, Mlingotini, Mbegani Juu, Mbweni, Ununio, Kunduchi, Kawe na Msasani. Maeneo mengine ni Kigamboni, Ufukwe wa Bamba, Kimbiji, Pemba Mnazi, Kibada, Nyamisati, Kisiju, Mkuranga, Ubungo na katikati ya jiji. Akitoa taarifa hiyo Dar es Salaam juzi, Kaimu Mkurugenzi Elimu kwa Mlipakodi, Diana Masala alisema kuwa bidhaa hizo, zimekamatwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Zilikamatwa katika msako uliofanywa na Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Idara ya Upelelezi Tanzania. Alisema kuwa bidhaa hizo zimekamatwa kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba mwaka huu kutokana na utaratibu wa kufanya doria na msako kwa pamoja katika maeneo ya mwambao wa mikoa ya Dar es Salaam

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Image
Mabusha ni hali ya kujaa maji kwenye mfuko wa pumbu. Hali hii hutokea kunapokuwa na mkusanyiko wa maji kati ya tabaka mbili za utando unaozunguka korodani. Inakadiriwa kuwa karibu asilimia moja ya wanaume wote kote duniani huathiriwa na tatizo hili. Kwa hapa nchini, tatizo hili ni maarufu sana maeneo ya mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, kiasi cha kuhusishwa na imani kadhaa. Mojawapo ya dhana iliyozoeleka miongoni mwa watu wa mwambao ni kuwa mabusha yana uhusiano mkubwa na unywaji wa maji ya madafu. Aidha, tatizo hili limekuwa likichukuliwa na baadhi ya watu kuwa ni hali ya kudhalilisha ingawa kwa wengine huonekana ni hali ya kuwa ‘mzee wa heshima’ au ‘umwinyi’. Ifahamike pia kuwa, tatizo la mabusha halitokei kwa wanaume watu wazima tu. Watoto wa kiume hususani katika mwaka wa kwanza (infants) pia ni waathirika wakuu wa tatizo hili. Kwa kawaida mabusha hayana maumivu na wala hayaleti madhara, isipokuwa kama yatapata uambukizi kwa sababu nyingine yeyote ile, hali inayowafanya

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI YA JAN 1,

Image
MAGAZETI YA LEO JUMAPILI YA JAN 1,2017..