TRA yanasa mali za mabilioni Dar
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata bidhaa za magendo, zilizoingizwa nchini kwa njia ya panya, ambazo zimeipotezea serikali kodi ya Sh bilioni 3.3 huku zikiwa na thamani ya jumla ya Sh bilioni 4. Aidha, imetaja maeneo korofi yanayotumika kuingiza bidhaa hizo kuwa ni Bagamoyo, Saadani, Mlingotini, Mbegani Juu, Mbweni, Ununio, Kunduchi, Kawe na Msasani. Maeneo mengine ni Kigamboni, Ufukwe wa Bamba, Kimbiji, Pemba Mnazi, Kibada, Nyamisati, Kisiju, Mkuranga, Ubungo na katikati ya jiji. Akitoa taarifa hiyo Dar es Salaam juzi, Kaimu Mkurugenzi Elimu kwa Mlipakodi, Diana Masala alisema kuwa bidhaa hizo, zimekamatwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Zilikamatwa katika msako uliofanywa na Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Idara ya Upelelezi Tanzania. Alisema kuwa bidhaa hizo zimekamatwa kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba mwaka huu kutokana na utaratibu wa kufanya doria na msako kwa pamoja katika maeneo ya mwambao wa mikoa ya Dar es Salaam