690 mbaroni kwa uhalifu wa mtandao
SERIKALI kupitia kitengo maalum cha uchunguzi wa jinai ya kimtandao, imefanikiwa kukamata watuhumiwa 690 kwa tuhuma za kufanya uhalifu wa mtandao. Watuhumiwa hao ni matapeli, wezi, waporaji wa simu za mkononi na wengineo wanaotumia mfumo wa intaneti kuibia watu wasiokuwa na hatia. Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Projestus Rwegasira alisema juzi jioni kuwa ofisi yake imekuwa ikikabiliana kikamilifu na wahalifu hao. Alisitiza kwamba wahusika wote wa vitendo hivyo, watakamatwa. Meja Jenerali Rwegasira alikuwa akizungumza katika mahojiano katika kipindi cha Tunatekeleza, kinachorushwa na Televisheni ya Taifa(TBC). Kwamba wizara yake kwa kushirikiana na vyombo vya serikali, inaandaa mashtaka dhidi ya watuhumiwa waliokamatwa na watafikishwa mahakamani. “Tunafanya kila juhudi kuzuia vitendo vya uhalifu wa kimtandao, tayari tumekamata baadhi ya watuhumiwa na watakabiliana na mkono wa sheria mahakamani,” alisema. Alisema serikali imeunda kitengo maalumu chini ya Wiz